Nchagwa Manga, mama mzazi wa Mkurugenzi
wa Kituo cha Michezo cha Alliance kilichopo jijini Mwanza, James
Bwire aliyefariki Januari 25, 2025, naye amefariki leo ljumaa Januari
31, siku ya kumuaga mwanaye
Akizungumza na Mwananchi leo ljumaa Januari 31, 2025,
Mwenyekiti wa Kituo cha Alliance, Stephano Nyaitati amethibitisha
kifo cha Nangwa
Nyaitati amesema kikongwe huyo amefariki asubuhi ya leo (ljumaa)
wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ye
Bugando, saa chache kabla ya kufanyika ibada ya kuagwa mwili wa
mtoto wake
Bwire alifariki Januari 25, 2025 saa 4 usiku wakati akipatiwa
matibabu katika Hospitali hiyohiyo ya Bugando, Mwanza baada ya
kuugua ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.
Licha ya kutokea kwa msiba wa kikongwe huyo, Nyaitati amesema
ratiba ya kumuaga na kumzika James Bwire, itaendelea kutekelezwa
<ama ilivyopangwa, kisha itaandaliwa ratiba nyingine kwa ajili yə
mazishi ya mama yake
0 Comments