USA yatoa onyo kwa Rwanda, yasema itakabiliwa na vikwazo isipokomesha Vita. Yamtaka Kagame kuondoa Majeshi yake Goma/Mashariki ya DRC

 


Marekani imehimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kuzingatia kuchukua hatua za kukomesha vikosi vya Rwanda na waasi vya M23 kuingia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huku mzozo huo ukiendelea kuongezeka.


Kaimu Balozi wa Marekani kwa UN Dorothy Shea hakuelezea kwa Baraza la Wanachama 15 ni hatua gani inaweza kuchukuliwa.

Lakini Baraza hilo lina mamlaka ya kuweka vikwazo.

"Tunataka kusitisha na kumaliza mapigano haraka iwezekanavyo. Rwanda lazima iondoe wanajeshi wake DRC. Rwanda na DRC lazima warudi kwenye meza ya mazungumzo na kushirikiana katika kupatikana kwa suluhisho endelevu na la amani," Shea aliiambia Baraza la Usalama.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waliandamana hadi Goma, mji mkubwa zaidi mashariki mwa Kongo, siku ya Jumatatu katika hali mbaya zaidi ya mzozo uliodumu kwa muda mrefu katika zaidi ya muongo mmoja.

Kongo iliishutumu Rwanda kwa kutuma wanajeshi wake mpakani, huku Rwanda ikisema mapigano karibu na mpaka yanatishia usalama wake, bila kuzungumzia moja kwa moja iwapo wanajeshi wake wako nchini Kongo.

Katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Therese Kayikwamba Wagner alitaka vikwazo kuwekwa dhidi ya viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Rwanda, kuwekewa vikwazo vya silaha, kupigwa marufuku kwa ununuzi wa maliasili za Rwanda na kuzuiwa kwa wanajeshi wa Rwanda kutoka kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: BBC

Pia soma

Post a Comment

0 Comments