Apple inaripotiwa kushirikiana na SpaceX kuunganisha
huduma za internet za satelaiti za Starlink kwenda moja
kwa moja kwenye iPhones. Watumiaji wa iPhone wataweze
kupata internet bila huduma ya mtandao wa simu
Kipengele hiki, kimeanza kufanyiwa majaribio katika
mfumo mpya wa ioS 18.3, kwa sasa utaratibu huu
unafanyika kama majaribio kwa watumiaji wachache wa
T-Mobile nchini Marekani
Mfumo huu utafanya kazi kiotomatiki pale mtumiaji akiwa
katika eneo ambalo hakuna mtandao lakini miaka ijayo
itakuwa ni huduma ya kawaida, hivyo watumiaji wa simu
wataweza kuamua kutumia mtandao wa Satelaiti au
mitandao ya simu.
Kwa sasa tayari watumiaji wa iPhone wanaweza kupata
nuduma za dharura kama vile kutuma meseji, kupiga simu
na kutafuta kifaa kilichopotea; lakini soon internet itakuwa
kwenye option
Unaonaje teknolojia hii?
0 Comments